Moto ni nini

Utangulizi

Kutokana na shughuli mbalimbali  za maendeleo ya binadamu, kuna umuhimu wa kuwa na elimu juu ya usalama wa moto na namna ya kukabiliana nao mara tu unapotokea kwa kuwa moto husababisha upotevu wa maisha,ulemavu na uharibifu mkubwa wa mali na hata  kusababisha watu kuishi katika hali kubwa ya umaskini.

SWALA LA USALAMA

Usalama wa maisha na mali  ni jukumu la kila mmoja wetu kwani moto unapotokea unasababisha vifo, ulemavu na kuteketea kwa mali kwa moto, Hiyvo elimu ni bora itolewe ili watu waweze kuchukua tahadhari.

MAANA YA MOTO

Moto ni mgongano/mpambano endelevu wa kikemikali ambao hutoa joto na mwanga kutegemea na hali ya mazingira na vitu vinavyoungua au kuwaka.

MAHITAJI YA MOTO

Ili moto uweze kutokea au kuwaka unahitaji vitu vitatu ambavyo ni:

Hewa ya Oksijeni (OXYGEN) ambayo ni 21% ya hewa yote katika uso wa dunia.

Chakula cha Moto (FUEL)– hiki ni kitu chochote kinachoweza kuwaka na kimegawanyika katika hali kuu tatu.

Joto (HEAT) – ni chanzo cha moto ambapo yaweza kusababisha na msuguano wa vitu mbalimbali au kiberiti ambayo  yaweza kusababisha moto.

Hivi vyote vinaitwa pembe tatu za moto.

CHAKULA CHA MOTO (FUEL)

Ni kitu chochote kinachoweza kuwaka,Vitu hivi vinapatikana katika hali tatu.

  1. Hali ya ugumu (solids) kama vile karatasi, nguo, majani na   plastiki n.k
  2. Hali ya vimiminika vinavyowaka (flammable liquids) kama vile Spritis, kerosine, Grease, Diesel, Alcohols.
  3. Hali ya Gesi (Gases) kama vile Hydrogen, Butane, Propane, Acetlyene,Coalgas n.k.

UKUAJI NA USAMBAJI WA MOTO

Kuna njia tatu ambazo moto unaweza kusambaa.

(a) Msafara (Convection)

Hewa inapopata joto hutanuka na kuwa nyepesi zaidi ya hewa  inayotuzunguka na huchanganyika  na gesi inayotoka kwenye moto na hupanda kwenda  juu kutengeneza msafara hivyohusaidia moto kusambaa toka sehemu za chini ya jengo hadi juu.

(b) Mnunurisho (Radition)

Katika njia hii joto husafiri kwakupitia maeneo wazi kama vile mionzi ya jua inavyosafiri na kutua jua ya uso wa dunia. Moto pia huweza kusambaa kwa njia hii kutokana na joto kusafiri toka kwenye kitu kilicho karibu na moto.

(a) Mpitisho (Conduction)

Katika njia hii joto husafiri kwa kupitia kwenye vitu vigumu kama vile chuma. Vyuma vilivyotumika ktk ujenzi wa  paa la jengo huchangia katika kusambaa moto.

NJIA AU MBINU ZA KUPAMBANA NA    MOTO

Kuna njia au mbinu tatu za kupambana na moto.

(a)Kupoza (COOLING)

Kupoza ambayo ni kitendo cha kushusha joto la kitu kinachoungua, kwa kutumia maji. Kitendo hicho kitaalamu kinaitwa Cooling

(b)Kufunika (Smothering)

Maana yake, ni kuzuia hewa ya oksijeni {oxygen} isifike kwenye vitu vinavyoungua. Inawezekana kufunika kwa kutumia vitu kama mapovu {foam}, poda kavu {dry powder}, blanketi {fire blanket}, mchanga mkavu ama kitu chochote kinachoweza kufunika moto bila chenyewe kuungua. Kitendo hicho kitaalamu kinaitwa Smothering.

(b)Kuondoa chakula cha moto, “Fuel”  (Starvation)

Maana yake, ni kuondoa vitu vinavyoungua katika vitu visivyoungua au kuondoa vitu visivyoungua katika vitu vinavyoungua. Kitendo hicho kitaalamu kinaitwa Starvation

Mtu akitumia njia moja wapo kati ya hizo tatu, atakuwa amevunja muungano wa pembe tatu za moto na moto utazimika.

MADARAJA YA MOTO

Kuna umuhimu mkubwa wa mtu yeyote kufahamu aina ya moto uliotokea ili aweze kuuzima kwa usalama na usahihi kwa kutumia kizimio sahihi ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na huo moto, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwaka au kusambaa kwenye sehemu zingine zilizosalama

Kuna madaraja manne ya moto ambayo ni kama ifuatavyo:

DARAJA LA KWANZA

Hili daraja linahusisha mioto yote yenye asili ya mimea kama vile makaratasi, nguo, mbao, kuni, majani, miti n.k.

Hapa kizimio sahihi ni maji

DARAJA LA PILI

Hili  daraja linahusisha mioto ya vimininika vinavyolipuka na kuwaka kama vile petroli dizeli mafuta ya taa, rangi ya mafuta, mafuta ghafi, mafuta ya kupikia n.k.

Kizimio sahihi cha mioto ya vimininika vinavyowaka ni fomu, unga mkavu, blanketi ya kuzimia moto, na mchanga mkavu

DARAJA LA TATU

Daraja hili linahusisha mioto ya gesi kama vile gesi asilia na gesi za viwandani mfano  Songas, Propen, Methen.

Kizimio sahihi ni kufunga valve ya gesi inayotoka kwenye mtungi uliohifadhi gesi.

Mara tu baada ya kufunga valve unaweza kutumia Unga mkavu  kwa kupulizia kwenye hewa inayo ungua. Unahitajika umakini wa hali ya juu.

DARAJA LA NNE

Mioto inayohusisha vyuma kama vile Aluminium, Zink, Koppa,makaa ya mawe n.k.

Kizimio sahihi ni ‘Unga mkavu.

Usitumie maji.

Kamishna Jenerali

Una Malalamiko?

Habari Mpya

Taarifa Kwa Umma

Kampeni Zetu

Instagram Feed

Wasiliana Nasi

Toa Ushuhuda wako