Vyeti na Ukaguzi

Ukaguzi na vyeti

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya ukaguzi kwenye vyombo vya usafiri na usafirishaji, na kutoa ushauri uwekaji wa vifaa vya kinga na tahadhari. Ukaguzi huu unafanyika kwa mujibu wa sheria namba 14 ya mwaka 2007 ikisomwa pamoja na kanuni ya Vyeti na Usalama wa moto Mwaka 2008 na marekebisho ya mwaka 2014 (Fire and Rescue Force Safety Inspections and Certificates Regulations of 2008 GN.106 and its Amendment GN 63 of 2014.)
Pamoja na kanuni ya tahadhari dhidi ya moto kwenye majengo ya mwaka 2015 (Fire and Rescue Force Fire Safety Precaution in Building Regulations of 2015 GN 516.)

Ukaguzi wa kinga/tahadhari za moto hufanyika wapi?

Ukaguzi wa usalama wa moto utafanyika kwenye majengo, na kwa yale majengo ambayo yanakidhi vigezo na mahitaji yote  muhimu ya usalama wa moto yatapatiwa Cheti cha Usalama wa Moto. Ukaguzi wa kinga na tahadhari za moto hufanyika katika sehemu zifuatazo;

 • Hoteli, nyumba za wageni, nyumba za sanaa, nyumba za wageni, hosteli na sehemu yoyote ile inayotoa huduma ya malazi yenye  uwezo
  wa  kulala zaidi ya watu sita
 • Hospitali na Taasisi zinazoyotoa huduma za matibabu.
 • Sehemu za  burudani, maagizo na  vilabu jamii na ushirika
 • Majengo ya taasisi za elimu na taasisi zingine za masomo, mafunzo au utafiti
 • Majengo ya taasisi ambazo ni kwa matumizi ya umma au wanachama tu ikiwa ni kwa malipo au vinginevyo
 • Majengo yanayotumika kama mahali pa kazi ambapo zaidi ya watu kumi kwa jumla wanafanya kazi kwa wakati mmoja
 • Mapomba ya gesi
 • Sehemu za kuzalisha na kutunza gesi
 • Migodi
 • Maeneo yanayozalisha umeme
 • Facilities used of gain storage and milling
 • Maeneo ya kuhifadhi wa vitu vya vinavyo
 • Eneo lolote lile ambalo kwa maoni ya Kamishna Jenerali ni linaweza kusababisha moto

Cheti cha Usalama wa Moto

Cheti cha ukaguzi wa usalama wa moto (Fire Safety Certificte) kinachotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji hutumika kama uhakikisho kwamba jengo, taasisi au ofisi fulani limekaguliwa kwa usahihi na ilionekana kufuata kanuni za moto za Nchini Tanzania

Cheti hutolewa kila mwaka baada ya ukaguzi kufanyika na taasisi husika kukidhi vigezo. Ukaguzi  inalenga  kutathmini na kupunguza hatari zinazoweza kusababisha  moto na kuhatarisha usalama wa maisha katika majengo.

Baada Ukaguzi  ripoti  ya marekebisho yoyote ambayo ni muhimu hutolewa . Marekebisho haya hutofautiana kulikana taasisi husika. Ukaguzi huo kunaendana na tozo ya ada ya Ukaguzi

Hatua za kufuata ili kupata cheti cha Usalama wa moto

 1. Maombi ya kupata cheti cha moto yanaweza kufanywa kwa Jeshi la Zimamot na Uokoaji.
 2. Tembelea Kituo cha Zimamoto katika wiliya ilipo ofisin yako, Hapo utapatiwa mkaguzi ambae atakuja kwenye ofisin yako na kufanya ukaguzi. Pia Jeshi la Zimamoto linaendesha zoezi la ukaguzi kila  siku
 3. Baada ya ukagauzi utapatatiwa namba ya malipo ili ufanaye malipo ya tozo ya dada ya Ukaguzi
 4. Pia utapatiwa ripoti na baada ya kukidhi vigezo utapatiwa cheti cha usalama wa moto

Vyombo vya Usafiri

Huduma hii ya ukaguzi wa vyombo vya Usafiri na Usafirishaji inatolewa bure. Ukaguzi huu unazingatia uwekaji wa vifaa vya uzimaji moto katika vyombo hivyo pamoja na utoaji wa elimu ya kinga na tahadhari ya moto kwa watumiaji.

Jeshi linatoa rai kwa wananchi wote kupeleka magari yao katika vituo vya Zimamoto vilivyopo karibu ili kupata huduma hii, HUDUMA HII NI BURE na ni kwa USALAMA WAKO MWANANCHI.

Iwapo utapata huduma hii kwa kutozwa fedha yeyote tafadhali wasiliana na Kamanda wa Mkoa husika, kwani ni kinyume na utaratibu..

Mambo ya kuzingatia kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri

Wamiliki wa vyombo vya usasafiri ndo wenye jukumu la kuzingakia usalama wa moto katika vyombo vya usafiri. Kila mmiliki wa chombo cha usafiri anapaswa kuzingatia yafuatayo;

 • All windows are not obstracted in anyway at all ti es when the vehicle is in use
 • The fire fighting facilities installed in the vehicle are maintained and kept in serviceable condition at all times
 • Any person employed to work has already receive instructions or trained on what to do in case of emergency
 • The vehicle does not carry hazardous material.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji