Huduma ya Matibabu ya Dharura
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya Huduma ya Matibabu ya Dharura ya masaa 24 Emergency medical Service (EMS), ambayo iko tayari kujibu dharura yoyote ya matibabu ndani ya Tanzania. Mwananchi akipata dharula ya matibabu Jeshi linatoa huduma ya gari la dharula ili mgonjwa aweze kufika hospitali haraka iwezekanavyo. Askari wetu wamefunzwa vizuri na pia wana vifaa vya kushughulikia dharura nyingi za matibabu.