Mhe. Rais Magufuli alizindua jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dodoma. Jengo hili lenye ghorofa tatu limejengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 2.656 kwa utaratibu wa ‘Force Account’ na ujenzi wake ulioanza Februari 2019 umekamilika Machi 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpandisha cheo DCP John Masunga kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 3, 2020
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Peter Mwambene (kushoto) akiwapatiwa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, kulia ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Elinimo Shang’a.